Here some review about ray c uchi, picture video you can get.
You can search in youtube too.

Inasemekana ndiye msanii wa kike mwenye mvuto kushinda wote Afrika Mashariki. Jina lake halisi ni Rehema Chalamila. Wapenzi wa muziki wake wanamtambua zaidi kwa jina Ray C. Ndio kwanza una umri wa miaka 25. Jina lake lilianza kuvuma alipokuwa mtangazaji redioni kabla hajaamua kuingia rasmi kwenye ulimwengu wa muziki,sio tena kama DJ bali muimbaji/mwanamuziki. Ingawa anasema angependa watu wausikilize na kuucheza muziki wake zaidi ya kuongelea uchezaji wake awapo jukwaani(viuno), ukweli unabakia kwamba Ray C ni mmojawapo wa entertainers wazuri jukwaani.Hivi karibuni BongoCelebrity ilifanya naye mahojiano yafuatayo. Katika mahojiano haya Ray C anazungumzia historia yake kimuziki toka utotoni mpaka alipo hivi sasa,mipango yake ya baadaye na kama lengo la BongoCelebrity anatoa ushauri kwa vijana wanaotaka kuingia kwenye fani ya muziki.Pia anaweka wazi swali je alishawahi kuolewa? Na nani?
BC: Wengi tunafahamu kwamba historia yako ya muziki ilianzia ulipokuwa unasoma katika shule ya Kabojja iliyopo nchini Uganda.Lakini kwa vyovyote vile hukuanza kuusikia muziki ulipokuwa nchini Uganda bali tangu utotoni.Unakumbuka ni wanamuziki gani uliwahi kuwasikia aidha sifa zao au muziki wao ulipokuwa mdogo? Je walikuwa na mchango wowote katika uamuzi wako baadaye wa kuingia kwenye muziki?
RAY C: Kama mtoto mwingine yeyote anayezaliwa nchini Tanzania, nilipokuwa mdogo nilikuwa napenda kusikiliza muziki. Wanamuziki wa hapa nyumbani ambao nakumbuka nilikuwa napenda kuwasikiliza ni wengi lakini wanamuziki kama Bi.Shakira (mwimbaji wa taarabu) na Remmy Ongala nilikuwa napenda zaidi kuwasikiliza.Nilikuwa napenda sana kumsikiliza Bi.Shakira kwa sababu nilikuwa napenda sana miziki yenye mahadhi ya taarabu hivi.
Lakini pia nilikuwa napenda sana kusikiliza nyimbo za kihindi na pia kuangalia sinema za kihindi. Nakumbuka utotoni nilipokuwa nikitoka tu shule nikifika nyumbani ni kuweka mikanda ya sinema za kihindi. Nilikuwa sio msikilizaji mzuri sana wa redio kipindi hicho. Nakumbuka nilichokuwa nakifanya wakati nikiangalia sinema za kihindi ni kwamba wanapofikia tu sehemu ya kucheza (unajua tena movie za kihindi,kila baada ya action fulani,muziki unafuata) nachukua kalamu na karatasi naandika wanachoimba kwa kiswahili,kama ninavyosikia. Ilifikia mahali ikawa mtu akiniambia niimbe wimbo fulani wa kihindi nauimba wote lakini bila hata kuelewa maana yake.Ingawa sikujua wakati huo,kumbe ndio taratibu nikawa najifunza uimbaji.Nadhani ndio maana hata hivi leo,ukisikiliza vizuri baadhi ya nyimbo zangu utasikia zina baadhi ya vionjo au mahadhi ya kihindi hivi.
BC: Kabla hujaamua kuwa mwanamuziki ulikuwa mtangazaji redioni au DJ. Huwa unamiss kazi yako ya utangazaji? Kama ndio unamiss nini?
RAY C: Ni kweli, wakati mwingine namiss utangazaji.Pengine simiss utangazaji kama kazi lakini namiss ile kuwa studio na kupiga nyimbo fulani fulani ninazozipenda. Pia namiss ule uhusiano unaokuwepo baina ya mtangazaji na wasikilizaji wake. Kama unavyojua baadhi ya wasikilizaji huwa wanatokea kupenda kipindi fulani kutokana na aidha aina ya miziki inayopigwa au mtangazaji mwenyewe. Kama utakumbuka wakati huo mimi nilikuwa ndio DJ pekee mwanamke nchini Tanzania. Kwa hiyo wakati mwingine namiss utangazaji lakini sema tu kwa sababu muda unakuwa hakuna na mambo ni mengi hivyo inakuwa hakuna jinsi.
BC: Ulipokuwa mtoto uliwahi kuota kwamba siku moja utakuwa msanii maarufu kama ulivyo hivi leo?
RAY C:Hapana sikuwahi kabisa kuota. Lakini nadhani kwa ujumla uanamuziki ndio ilikuwa ndoto yangu maishani ila nilikuwa sijui tu nianzie wapi. Hii inatokana na ukweli kwamba nilikuwa napenda sana mambo ya muziki kama nilivyosema hapo juu.Yaani mimi mwenyewe kuna wakati nashangaa kwamba nipo hapa nilipo hivi sasa.
BC: Kuna mtu yeyote unamkumbuka alikushawishi uingie kwenye muziki?
RAY C: Kuna watu wawili watatu ambao walinishawishi kuingia katika muziki.Lakini sana sana ni Ruge Mutahaba ambaye wakati huo ndiye aliyekuwa meneja wangu pale Clouds FM. Nakumbuka mara nyingi kila baada ya kumaliza kufanya kipindi changu redioni alikuwa akinisikia nikiimbaimba kwenye corridors za pale ofisini na ndipo akanishauri kama ninapenda kuimba na ningependa kurekodi basi nifanye mazoezi zaidi ya uimbaji, nitafute mtu aniandikie wimbo au niandike mwenyewe niingie studio kurekodi japo single moja kwanza na kisha kama itakuwa nzuri basi yeye angenisaidia kurekodi albamu nzima.
Mtu wa kwanza kuniandikia wimbo akawa ni Patricia Hillary wa JKT Taarabu,yeye ni mwanamuziki wa taarab. Nilikuwa nataka niingie kwenye viwanja hivyo .Aliniandikia wimbo wa Mapenzi Yangu ambao ndio ulikuwa wimbo wangu wa kwanza kutoka kwenye albamu yangu ya kwanza. Wakati huo Ruge tayari alikuwa na kampuni ya Smooth Vibes ambayo ilikuwa na wasanii kama vile Banana Zoro, Lady Jay Dee na wengineo.Huo ndio ukawa mwanzo wa safari yangu hii ya muziki.


